Ugomvi wa Mke na Mume wasababisha Nyumba kubomolewa

Adimin
0

 Taharuki na malumbano vimeibuka katika Mtaa wa Mabibo Wilayani Ubungo Jijini Dar es salaam baada ya nyumba zaidi ya nne na fremu zaidi ya tano kuvunjwa na Watu waliotumwa na aliyeuziwa eneo hilo ambapo Wahusika wamesema uvunjwaji huo umefanyika licha ya Mahakama kutoa zuio kuwa eneo hilo halipaswi kuuzwa wala kubomolewa kwakuwa lina mgogoro kati ya Mume na Mkewe wa zamani.


Eneo hilo ni mali ya Mzee Mwinjuma Mazige na Mkewe wa zamani Aziza Selemani ambao walioana na kuishi kwa muda mrefu wakiwa na Watoto saba, kabla ya baadaye Mzee huyo kuoa Wake wengine wawili na kumuacha Mke na Familia na kudaiwa kuanza kuuza maeneo wanayomiliki bila kumpa mgao Aziza ambaye walitafuta mali pamoja na kupelekea Aziza kufungua kesi na Mahakama kuweka zuio kuwa eneo la Mabibo lisiuzwe.

Familia inadai kama sio Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuingilia kati kwa kuwapigia simu Askari katika eneo hilo na kuwataka wazuie bomoabomoa hiyo huenda wangevunja nyumba zote hadi ambayo Familia inaishi ambapo @AyoTV_ imemtafuta DC Bomboko kwa njia ya simu na kukiri ni kweli alipopigiwa kuwa nyumba zinabomolewa akaagiza zoezi lisitishwe na amri ya Mahakama iheshimiwe.

Bi. Aziza amenukuliwa akisema “Mama Samia nisaidie Mwanamke mwenzako napata aibu, naombeni Serikali mnisaidie, zuio hawakuliona na wamevunja, nikakaa ndani nikasema wavunje wakikuta maiti wanatoa kwenda kuzika, chanzo wenzangu kuolewa, Mume wangu alioa Mke mwingine akaona hajapata Mtoto akaoa Mke wa tatu ambaye ni Mdogo wa yule Mke wa mwisho kwahiyo Wake zake wawili ni Ndugu Baba mmoja Mama mmoja ndio wameenda kupiga picha na kutia saini eneo liuzwe, wamesema leo mwisho wameacha gari kesho nisipoondoka wanavunja”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top