Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Ramadhan Tembo Mwakilasa (28) na Mariamu Charles Mwashambwa (28) wote wakazi wa TEKU viwandani Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Chloy Ramadhan (04) kwa kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili huku sababu ikitajwa kuwa ni baada ya mtoto huyo kujisaidia kwenye nguo alizokuwa amezivaa.
Polisi wameeleza kuwa Novemba 25, 2024 saa 2:00 usiku huko Mtaa wa TEKU viwandani Jijini Mbeya, mtoto Chloy Ramadhan (04) alifariki dunia baada ya kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi aitwaye Ramadhan Tembo Mwakilasa (28) akishirikiana na mama yake wa kambo aitwaye Mariamu Charles Mwashambwa (28) wote wakazi wa TEKU viwandani