Billioni 53 za hati fungani kuboresha huduma ya maji mkoani Tanga

Adimin
0

 Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Hamidu Aweso(MB) ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) kwa ubunifu uliofanyika wa uwekezaji wa Hatifungani ya Kijani (Tanga Water Green Bond) itakayofanikisha utekelezaji wa miradi ya maji  katika maeneo ya Jiji la Tanga pamoja na Miji ya Muheza na Mkinga.

Akizungumza wakati akikagua utekelezaji wa Miradi ya Maji Mkoani Tanga, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema kuwa Mkoa wa Tanga umekuwa kielelezo katika Sekta ya Maji nchini kutokana na utendaji kazi mzuri wa kuboresha hali ya upatilanaji wa huduma kwa wananchi Tanga.



Sambamba na hilo Waziri Aweso pia amempongeza Mkurugenzi Mtendaji TANGA UWASA Mhandisi Geofrey Hilly kwa ushirikiano wake mzuri na viongozi wa serikali katika Mkoa wa Tanga na kuhimiza kuendeleza mashirikiano ili kufikia lengo la kufikisha huduma bora kwa Wananchi, pamoja na kusisitiza ukamilishaji wa mradi kwa wakati ili kuboreshaji upatikanaji wa Maji kwa uhakika.


Mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji maji Tanga Awamu ya Tatu unajumuisha  kuongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji maji kutoka lita za ujazo 45,000 hadi 60,000 kupitua uboreshaji wa kituo cha kusukuma maji cha Mabayani, Mtambo wa Kutibu Maji wa Mowe, uendelezaji wa mtandao wa mabomba, uboreshaji wa miundombinu chakavu, ufungaji wa Mita 10,000 za malipo ya kabla (Pre-paid Water Meters) na uboreshaji wa shughuli za uhifadhi wa Mazingira.


Mradi huu unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2025 na kukamilika kwake kunaenda kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wakazi wa Wilaya tatu zenye wakazi zaidi ya 469,000.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top