𝗨𝗝𝗨𝗠𝗕𝗘 𝗪𝗔 𝗛𝗔𝗠𝗭𝗔 𝗔𝗟𝗜𝗘𝗡𝗔𝗦𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗞𝗜𝗙𝗨𝗦𝗜 𝗛𝗨𝗞𝗢 𝗞𝗔𝗥𝗜𝗔𝗞𝗢𝗢....!!!

Adimin
0

“Brother nakufa, nahema kwa tabu, vumbi ni zito. Giza limetanda. Sioni chochote mbele yangu.”Anasema:



“.....simu yangu ina asilimia 6 tu, muda wowote itazima chaji. Nimebanwa na kifusi huku chini kaka, naomba ufanye kitu, sitaki kufa, kaka. Naogopa sana.”

Mguu wangu umebwa na kitu kama jabali zito, nashindwa kabisa kujinasua hapa, tangu asubuhi nimelala, siwezi kugeuka, nahisi, kuchoka, maumivu hayaelezeki labda nimevunjika, maana mguu unauma sana. Mwili unakosa nguvu.

“Dalili za uhai ni ndogo kuliko kifo, mbaya zaidi nakufa taratibu, kwa maumivu makali...nimechoka sana, najisikia vibaya, nashikwa na kichefu chefu, nikivuta pumzi, navuta vumbi inayonipa kikohozi. Joto ni Kali na hewa ni nzito sana.


Awali nilidhani muda si mrefu nitaokolewa lakini Sioni dalili zozote za kufikiwa, nakufa Mimi jama, nikiwa Sina chochote nilicho acha kwa ajili ya watoto wangu.

Msaidieni mama Yasir, wasaidieni watoto wangu, wasaidieni tafadhali. Fanya kwa ajili yangu kama nitakufa....

Mwambie mama Yasir nampenda sana,

Nilipambana Kwa ajili ya familia, anajua hilo ila jitihada hazishindi kudra.

Ana maliza kwa kusema hivyo Bwana Hamza ambaye ni Muhanga wa Ajali ya kuporomokewa na Ghorofa huko Kariakoo.

INAUMIZA SANA KWA KWELI, TUWAOMBEE NDUGU ZETU.😭💔
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top