Na Stephano Mango, Mbinga
MKURUGENZI Joseph Kashushura amewapongeza Waganga Wafawidhi wa vituo ya kutolea huduma za afya vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kuimarisha usimamizi katika vyanzo vya mapato ya ndani katika vituo hatua iliyopelekea kuongezeka kwa mapato na upatikanaji wa huduma za afya.
Pongezi hizo zimetolewa jana katika Kikao cha kutoa tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe katika kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Baadhi ya viongozi hao ambao wamepongezwa ni Mganga Mfawidhi Zahanati ya Myau Amiri Kahurananga ambapo makusanyo ya kituo yameongezeka kutoka 822,236.25 hadi kufikia 5,074,321 sawa na
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Dkt. Salum Bundala ambapo makusanyo katika Hospitali hiyo yameongezeka kutoka 32,625,000 hadi kufikia 155,177,937 sawa na 373%.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Amani Makolo Joseph Washawasha, makusanyo yameongezeka kutoka 1,811,516.41 hadi kufikia 3,933,417.00 sawa na 217.13%.
Pamoja na pongezi hizo Mkurugenzi Kashushura amewataka Waganga Wafawidhi kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo wanavyovisimamia ili fedha inayopatikana itumike katika kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya kwa jamii.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki hao Joseph Washawasha amebainisha kuwa mafanikio hayo yametokana na kujituma,uzalendo pamoja na kutimiza majukumu yao kikamilifu.