Wananchi wahamasishwa kupata elimu ya Nishati safi ya Kupikia

Adimin
0

Na Stephano Mango, Songea 

MAADHIMISHO ya Siku ya UKIMWI Duniani yameendelea kufanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea, ambapo kilele cha sherehe hizi kitakuwa ni Disemba mosi na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philipo Mpango 

Sherehe hizi zinajumuisha shughuli mbalimbali za kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI, pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma za afya. Maadhimisho haya yanajumuisha maonyesho ya huduma za afya, mashirika ya kijamii, na kampuni mbalimbali zinazoshiriki katika kukuza ustawi wa jamii.


Katika maadhimisho haya yanayoendelea majimaji nilipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali, likiwemo banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Ruvuma. 


Banda hili limekuwa kivutio kwa wananchi wengi, ambapo wateja wamepokelewa na msaidizi wa afisa huduma kwa wateja, Emma Ulendo ambaye alitoa elimu kuhusu huduma za umeme. 


Emma alisisitiza umuhimu wa wananchi kutembelea banda hilo ili kupata huduma za dharura, kupata kuomba maombi mapya ya umeme, aidha Alisema yuko tayari kujibu maswali yoyote yanayohusiana na umeme.


Kwa sasa, jamii inahitaji huduma za nishati safi na kidigitali, na TANESCO imetoa fursa hii kwa wateja kutembelea banda hilo ili kupata taarifa na huduma muhimu. 


Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora za nishati na pia wanaelimika kuhusu matumizi ya umeme katika nyanja mbalimbali za maisha yao ya kila siku.

MWISHO

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top