Na Linda AKyoo
Vijana askari 80 wa Jeshi la Akiba (Mgambo) wamehitimu mafunzo yao ya miezi minne yaliyofanyika katika kata ya Bombo, Tarafa ya Gonja Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, askari hao wamekula kiapo cha utii kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,tayari kufanya kazi kwa kujitolea kulitumikia Taifa kama walinzi wa usalama wa raia na mali zao.
Aidha amewasisitiza askari hao kwamba Pamoja na wajibu wao wa msingi kwnye masuala ya usalama, askari hao ni kiungo muhimu kuhamasisha uzalendo kwenye jamii, kuunganisha Serikali na jamii hasa panapohitajika ushiriki wa raia katika shughuli za kijamii za kujitolea Pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo hasa nguvu kazi.