Kwa mara Nyingine Makete inaenda kuandika historia nyingine baada ya kuandaliwa kwa Tamasha la Mbuzi Choma ambalo litawahusisha wananchi wote watakaofika eneo la Soko la Ngiu Makete Mjini Kula Nyama kwa Uwezo wako bila Kulipia chochote.
Akizungumza Mratibu wa Tamasha hilo lililopewa jina la FUNGA MWAKA NA MBUZI CHOMA MAKETE 2024 Award Mpandila amesema lengo kuu ni Kuwahamasisha wananchi wa Makete Kupenda kurejea nyumbani, Kuoneshana Upendo ,kubadilishana mawazo ya maendeleo na kufahamiana kwa lengo la Kuijenga Wilaya ya Makete yenye Maendeleo.
Amesema Kwenye siku ya Disemba 31,2024 kunatarajiwa kuchinjwa Mbuzi 16 na kwa wale ambao hawali mbuzi basi wameandaliwa kondoo na kuku ambapo mpaka Disemba 29 2024 maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90%.
Endelea kufuatilia Idawa Media kwa Updates Zaidi kuhusu Tamasha la Kula Mbuzi Choma Makete 2024 RUDI NYUMBANI KUMENOGA.