Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linawashikilia watu Saba kwa kosa la kusambaza taarifa za vitisho kwa viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa kijiji kwa kubandika mabango kwenye ofisi zao na kuwataka kutozifungua ofisi hizo na kuwatishia kuwaua.
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa Polisi Mkoani humo Mahmoud Banga amesema sambamba na kikamatwa watuhimiwa hao uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.