Wadau wa Maendeleo Wilayani Makete, waishio Dar es Salaam, Desemba 23, 2024, wamekabidhi Vifaa Tiba pamoja na Elimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, vyenye thamani ya shilingi milioni 140.
Akizungumza wakati wa Kukabidhi Vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo waishio jijini Dar es Salaam, Ndg. Dkt. Toba Nguvula, amesema kuwa, huo ni mwanzo tu wa kuijenga Makete mpya, na kwamba watahakikisha wanatatua changamoto ambazo zitakuwa juu ya uwezo wao.
Aidha, Dkt. Nguvila, amewataka watumiaji wa Vifaa hivyo, kuhakikisha kuwa wanavitunza ili viweze kudumu kwa muda mrefu, na kwamba wao watakuwa na kazi kujazilizia pale penye uhitaji kutegemea na maombi ya wanamakete.
"Wilaya ya Makete, imebarikiwa kuwa na watu wenye uwezo pamoja na nafasi kubwa sehemu mbalimbali pamoja na Wafanyabiashara wakubwa ambao tukiwaweka kwa pamoja naamini Makete hii itabadirika" Alisema Dkt. Nguvila.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma S. Sweda, akiongea kwa njia ya Simu kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, amewashukuru wanamakete hao kwa kuamua kurudi nyumbani ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya pamoja na Elimu.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Y. Fungo, akishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Makete, amesema kuwa watahakikisha wanatunza Vifaa hivyo, ili viwe na tija kwa vizazi vyote, sambamba na kuwaomba waendelee kuishika mkono Wilaya Yao kwakuwa Maendeleo ni Mapambano.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amesema kuwa, msaada huo uliotolewa na na Wadau hao ni matokeo chanya ya ishirikiano Mzuri uliopo katika ya wanamakete pamoja na Uongozi mzima wa Wilaya ya Makete.
Ikumbukwe kuwa, Wadau wa Maendeleo waishio jijini Dar es Salaam, wametoa msaada wa Vifaa Tiba pamoja na Elimu, ili kuhakikisha Wilaya ya Makete inaboreka katika Utoaji wa huduma muhimu kwa Wananchi.
![]() |
Vifaa vilivyotolewa na Wadau wa Maendeleo |
![]() |
Toba Nguvila RAS wa Mkoa wa Daresalaam na Mdau wa Maendeleo Makete |
![]() |
William Makufwe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Makete |
![]() |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Bw Christopher Fungo |