Watumishi TRA wajeruhiwa wakidhaniwa Watekaji

Adimin
0

 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na Watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, Dar es salaam December 05, 2024 usiku.


Taarifa iliyotolewa usiku huu na TRA imenukuliwa kama ifuatavyo “Kadhia hii imetokea baada ya Watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba

T229 DHZ aina ya BMW X6 lililoingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za Serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”


Download App ya Kupata ODDS bure kila siku <HAPA>


“Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa, Mamlaka ya Mapato Tanzania inawapa pole Watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii na kuwaombea wapone kwa haraka, Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top