Afungwa Jela kwa kutumia sare za JWTZ kwenda kutongoza bila ruhusa

Adimin
0

Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa.


Hukumu hiyo imetolewa Januari 07, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.12.2024 huko kijiji cha Kasisa, Wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani Januari 07.2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ni mzito na haukuacha shaka lolote.

Hata hivyo, mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetetea kwa nini asipewe adhabu; aliomba mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na alivaa ili akubaliwe na mchumba wake.

"Mhe. Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonesha mchumba wangu kuwa mimi ni Askari ili asinikatae," aliomba Rajabu.

Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu Kisoka na kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya Rajabu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top