Makonda ampiga spana Mbunge Gambo mbele ya wapiga kura wake

Adimin
0

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda  Januari 06, 2024 amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Mashaka Gambo, kuachana na siasa za uchonganisha na badala yake ahudhurie vikao vya Mipango ngazi ya Halmashauri na vya ngazi ya Mkoa ili kujadili pamoja kuhusu changamoto na suluhu za masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa wa Arusha.


Mhe. Makonda akiambatana na Waziri wa ujenzi Abdallah Ulega, ametoa kauli hiyo  wakati wa Ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa inayojengwa kwa kiwango cha lami, akisema kutohudhuria vikao hivyo na badala yake kusubiri kuwasilisha changamoto zao kwa Viongozi wa kitaifa wanaofika mkoani hapa kwa ziara za kikazi ni uchonganishi usiokubalika na unaokwamisha shughuli za maendeleo.

Makonda aliyeambatana na Waziri wa Ujenzi na Watendaji wakuu wa Wizara hiyo kwenye kukagua miradi mbalimbali ya Ujenzi Mkoani Arusha, aliwaambia Wananchi wa Ilboru, Arumeru kuwa masuala mbalimbali yanajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na maelekezo ndani ya Vikao mbalimbali vya mipango vinavyoitishwa ngazi ya Halmashauri na ngazi ya Mkoa na ni wajibu wa kila Kiongozi husika kuhudhuria ili kuwa na kauli ya pamoja na utekelezaji wa pamoja kwenye masuala ya maendeleo ndani ya Halamshauri na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top