Mapenzi achoma nyumba aliyopanga mpenzi wake wivu wa Mapenzi watajwa

Adimin
0

 Mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Lino anadaiwa kuchoma moto nyumba aliyopanga mpenzi wake katika mtaa wa Idundilanga halmashauri ya mji wa Njombe na kukimbia huku chanzo kikidaiwa kwamba ni baada ya ugomvi uliotokea baina yake na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Janeth Ngimbudzi baada ya kumkuta kazini kwake akiwa amekaa na mwanaume mwingine.



Akizungumza na kituo hiki Ajentina amesema jana January 11 majira ya saa nne usiku ulitokea ugomvi baina yake na mpenzi wake aliyempata kwa muda wa wiki tatu sasa ambapo alifika kazini kwake sehemu ya kuuzia nyama na kumkuta mwanaume mwingine anayedaiwa kuwa ni mteja wake aliyekuwa amekaa naye jikoni na kuanzisha ugomvi uliomfanya mteja kukimbia eneo hilo hali iliyopelekea mwanaume kwenda kuchoma nyumba yake.

"Kulikuwa kuna mteja amekaa jikoni alipofika akasema huyu mteja anatafuta nini jikoni mimi nikamwambia huyu ni mteja tu kama wengine akaanza kumpiga nikaamua na yule mteja akakimbia alipomfukuza na kumshindwa akatoka pale na kuja nyumbani akawasha nguo zikadaka moto juu na yeye akakimbia,wakati amefika hapa watoto wanamjua walimuona kazini wakajua sio mgeni kwa hiyo alivyoomba funguo wakampa akanyosha chumbani na kuwasha moto"amesema Ajentina

Nao baadhi ya majirani akiwemo Thadei Lugome pamoja na January Mtega wanasema majira ya usiku walisikia kelele na kufika eneo la tukio ili kuokoa mali zilizokuwa ndai huku pia wakipiga simu kwa jeshi la zima moto na uokaji waliofika mapema na kusaidiana kuudhibiti moto huo ambapo pia wameelaani kitendo hicho cha kikatili kwa kuwa kingepelekea vifo vya watu waliokuwa wamelela kwenye nyumba hiyo.

Mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Njombe Joel Mwakanyasa amesema walifanikiwa kufika eneo la tukio majira ya saa nne na dakika ishirini usiku mara baada ya kupata taarifa ya kuungua nyumba hiyo kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kuuzima kwa muda mfupi ambapo tathmini iliyofanyika wamebaini kuwa moto huo umetokana na mafuta.

"Pale pana nyumba yenye vyumba nane vya wapangaji na vilivyoungua ni vyumba vitatu na kwa bahati mbaya huyu mpangaji ambaye aliunguliwa hatuweza kuokoa kitu chochote na mpangaji wa pili viliokolewa lakini vilikuwa vimeungua kwa sababu moto ulikuwa wa kasi sana kwa hiyo tuliabaini mchomaji alitumia kilipuzi cha haraka"amesema Mwakanyasa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top