Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki wapewa Angalizo Mbinga

Adimin
0

Na Stephano Mango, Mbinga 

WAANDISHI  wasaidizi pamoja na  waendesha  vifaa vya  Bayometriki  Jimbo la Mbinga Vijijini wametakiwa kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa weledi huku wakizingatia sheria na miongozo iliyopo katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga  kura.



Wito  huo umetolewa na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mbinga Vijijini  Paschal Ndunguru wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kumudu  la wapiga kura kwa  Waandishi wasaidizi pamoja na  Waendesha  vifaa vya Bayometriki 

Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mbinga Vijijini  Paschal Ndunguru akizungumza na washiriki wa Mafunzo hayo


Ndunguru alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea weledi na ufahamu kuhusu hili zoezi lililopo mbele yenu, sasa basi tuhakikishe tunatumia umahiri katika kufanikisha zoezi hili" Amebainisha


Sambamba na hilo amewataka kuzingatia muda elekezi  wa kufungua vituo vya kujiandikisha   ili ifikapo saa mbili asubuhi wananchi waanze kupata huduma na kupata muda wa kuendelea na majukumu yao ya kila siku.


Aidha amewataka kutunza vifaa ambavyo vitatumika wakati  wote wa zoezi hilo akisisitiza kuwa Serikali imetumia fedha nyingi katika unuuzi wa vifaa , hivyo  kila mmoja ana wajibu wa kutunza na kuhakikisha usalama wa vifaa unakuwepo


Kwa upande wake Afisa kutoka Tume  Huru  ya  Taifa ya Uchaguzi  Nicholaus  Natay amewataka maafisa hao kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili  kurahisisha na kuhakikisha  utekelezaji wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linakamilika bila changamoto yoyote.


Naye Afisa Uchaguzi  kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga  Andrew Mbunda ametoa rai kwa washiriki hao kuwa na nidhamu na kutoa huduma bora   kwa wananchi wanaokwenda kuwahudumia na kuepuka mazoea  katika utendaji kazi.


Akizungumza kwa niaba ya washiriki hao Mwandishi msaidizi  ambaye pia ni mwenyekiti wa mafunzo hayo  Elizabeth Banzi ameahidi kuwa watazingatia maelekezo yatakayotolewa na  kufuata miongozo  wakati wote wa utekelezaji.


Mafunzo haya yanafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 9 hadi10 Januari 2024 na zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoa wa Ruvuma litaanza rasmi tarehe 12 hadi 18 Januari 2024.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top