CBWSO watakiwa kutenda kazi kwa weledi kuisaidia serikali

Adimin
0

 Watendaji wa CBWSO wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kufanikisha mipango ya serikali katika kuwahudumia wananchi chini ya RUWASA.


Kauli hizo zimetolewa Februari 19, 2025 na viongozi mbalimbali katika semina iliyozikutanisha kamati tendaji za CBWSO kwa tarafa za Ukwama na Lupalilo chini ya Wakala wa maji na Usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA).

Robert Kato ni Afisa wa TAKUKURU wilayani Makete amesisitiza suala la kufuata sheria pamoja na uadilifu kwa manufaa ya miradi ya serikali hasa iliyo chini ya RUWASA sanjari na kuepuka vitendo vya rushwa ili CBWSO ziweze kupiga hatua.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Makete Mhandisi Innocent Lyamuya amesisitiza watendaji wa CBWSO kufanya kazi zao kwa weledi ili kuiwakilisha vema Taasisi hiyo huku akiwataka kuanza kupanda miti rafiki kwenye vyanzo vya maji kuelekea kilele cha wiki ya maji Machi 22 kama walivyoazimia katika semina hiyo.

Beauti Sileke ni Afisa Maendeleo ya jamii wa RUWASA wilayani Makete wakati akitoa mada yake kwa watendaji hao amewataka kufuata ngazi pindi zinapotokea changamoto za kiutendaji na kuacha tabia ya kukaa na changamoto zilizo juu ya uwezo wao zinazoletwa kwao na wananchi.

Cosmas Kaloa,Chesko Kitumbika,Lusiana Mbwilo pamoja na Yohana Ntulo ni baadhi ya wanufaika wa semina hiyo wameshukuru kwa mafunzo na kutoa maoni yao hasa kwenye eneo la kushirikiana miongoni mwa watendaji hali iliyoungwa mkono na meneja wa RUWASA wilaya ya Makete.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top