Jamaa Njombe ajiua baada ya kuambiwa mtoto si wake

Adimin
0

 Mwili wa kijana Justine Mbaga mwenye umri wa miaka 28 ambaye amefariki dunia  Februari 11,2025 ikidaiwa ni kwa kunywa sumu baada ya kupewa taarifa kuwa mtoto aliyekuwa anamhudumia si wake, umezikwa  katika makaburi ya Magegele yaliyopo Halmashauri ya mji Makambako.



Taarifa zinaeleza kuwa siku ya jumapili Februari 9,2025 familia ya binti ya aliyekuwa naye kwenye mahusiano walimwita Justine Mbaga, na familia yake na kumweleza kuwa mtoto ambaye alikuwa anamlea si wake, jambo ambalo lilipelekea kuathirika kisaikolojia na kuchukua uamuzi huo.

Baadhi ya majirani wa Justine Mbaga wamesema kifo cha mpendwa wao kimewaacha na majozi mazito kwani alikuwa ni kijana mwenye maadili mema.

Ratifa kibiki ni, mama mzazi wa binti mwenye mtoto huyo anayedhaniwa ni mtoto wa Justine Mbaga akizungumza na El olama fm amesema waliamua kumuita Justine Mbaga na Familia yake na kuwaeleza kuwa mtoto huyo si wao kwani aliona si busara Justine aendelee kulea mtoto ambaye si wake.

Aidha Mama huyo amesema binti yake alikuwa tayari kurejesha gharama za matunzo ambazo Justine Mbaga alizitumia kumlea mtoto huyo ambazo ni 850,000/=.

Diwani wa kata ya kitisi Nevy Sanga na mtendaji wa mtaa wa Kisingire,wameiasa jamii iache tabia ya kuchukua sheria mkononi hasa inapojitokeza changamoto yoyote kwenye maisha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top