KILO 380 ZA SUKARI ZAKABIDHIWA KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI 38

Adimin
0

Na Stephano Mango, Mbinga 

MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga  Joseph Kashushura ametoa tuzo (fedha taslimu)  kwa shule za Sekondari zilizofanya vizuri katika Mtihani wa kidato cha nne na kidato cha pili mwaka 2024 pamoja na kukabidhi  kilo  380 za sukari kwa shule za Sekondari za Serikali 38 ikiwa ni motisha kwa walimu katika ujifunzaji na ufundishaji.



Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika hafla ya utoaji wa tuzo za taaluma kwa shule za Sekondari  zilizofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha pili na Kidato cha nne mwaka 2024.


Pamoja na tuzo hizo Mkurugenzi amewataka walimu hao kutimiza majuku yao ya ufundishaji ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata umahiri na weledi.


" Tuzo hizi ni motisha katika kuboresha Elimu katika Halmashauri yetu sisi ambao hatujapata tujitahidi tupambane na wale ambao leo mmepata ongezeni spidi" Amesema



Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Rashid Bundalah ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 3,522 ikiwa 1,368 wavulana na 2,154 wasichana  kutoka katika  shule 49  walifanya Mtihani wa Upimaji Kitaifa  Kidato cha pili  mwezi Novemba  2024.


Aidha watahiniwa wapatao 2,205  ikiwa 893  wavulana na 1,312 wasichana  kutoka katika  shule 46  walifanya Mtihani wa  Taifa  Kidato cha nne  mwezi Novemba  2024.


Ili kuinua  ufaulu na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi  Bundalah amethibitisha kuendelea kufuatilia shughuli za ufundishaji na ujifunzaji na kuchukua hatua stahiki kwa walimu  wasiotimiza majukumu yao pamoja na kuwachukulia hatua  watu wanaosababisha  wanafunzi kukatisha masomo.


Kwa upande wake mwalimu Athanas Mbele  Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ameeleza tukio hilo ni deni  kwao katika kuhakikisha  wanainua ufaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Mwisho

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top