Sababu Yanga Kumtimua Kocha ni hii

Adimin
0

 Klabu ya Yanga SC imemtangaza Miloud Hamdi mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa kuwa kocha wake mpya akichukua mikoba ya Sead Ramovic ambaye anaondoka klabuni hapo baada ya kuvunja mkataba na kocha Mjerumani huyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.


Taarifa ya leo Februari 04, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa, Kocha Hamdi mwenye uzoefu mkubwa wa kufundisha soka akiwa amefanya kazi barani Ulaya, Asia na Afrika, anaungana na timu mara moja kuanza majukumu yake mapya.

Kocha huyo mbali na uzoefu alionao, pia ana mafanikio makubwa katika soka la Afrika akishinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa 2015-2016 akiwa na USM Alger.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top