Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Jumanne Machi 18.2025 kimemueleza Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusiana na msimamo wake wa 'No Reform, No Election' unaolenga kushinikiza mageuzi makubwa ya mifumo ya uchaguzi nchini, na kwamba endapo mageuzi hayo hayatafanyika basi chama hicho kupitia 'nguvu ya umma' kimejipanga kuzuia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu
Akizungumza na wanahabari nje ya viunga vya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa muda mfupi baada ya kutoka kwenye ofisi hizo, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema viongozi wa chama hicho wamelazimika kufika kwenye ofisi hizo kufuatia wito walioupokea hivi karibuni ambao pamoja na mambo mengine uliwataka kufika hapo ili kueleza wanamaanisha nini wanaposema 'No Reform, No Election'
Kupitia kikao hicho kilichochukua zaidi ya saa nne, Mnyika amesema viongozi wa CHADEMA wameieleza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa kauli hiyo hawajaitoa kwa bahati mbaya kwani kwa muda mrefu nchini kumeshuhudiwa chaguzi ambazo zisizokuwa huru na haki zisizoheshimu maoni ya wananchi wanayotoa kupitia masanduku ya kura, na kwamba mara zote imeelezwa na wadau mbalimbali kuwa mwarobaini wa yote hayo kufanyika kwa mageuzi ya mifumo ya uchaguzi ikiwemo kupatikana na Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, jambo ambalo linaonekana kupigwa chenga na watawala (Serikali na CCM)
FULL VIDEO YA CHADEMA HII HAPA👇👇👇👇
"Sisi (CHADEMA) tunaamini baada ya kutuita na sisi kuitikia wito wao, sasa wanapaswa kuyachukulia kwa uzito ili na wao (Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa) wawe na mchango kama wadau wengine tuliokutananao, mchango wa kuwezesha kufanyika kwa mageuzi na mabadiliko kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025, bila mabadiliko hakuna uchaguzi (No Reform, No Election) tunaamini jambo hili linapaswa kukubalika na wadau wote" -Mnyika
Hata hivyo, Mnyika amesema taasisi hizo mbili (CHADEMA na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa) baada ya kikao hicho wanatarajia kukutana tena hivi karibuni kwa mazungumzo mengine, lakini wakati hayo yakiendelea chama hicho kimeendelea kusisitiza msimamo wake uko palepale na hautabadilika na kwamba hivi karibuni watazunguka kuwaeleza wananchi...