Kamati ya siasa Makete wakagua miradi ya maendeleo,watoa neno

Adimin
0

 Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi, CCM, Wilaya ya Makete Machi 5,2025, imekagua Utekelezaji wa Ilani ya chama hicho, katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete, ambapo imeridhishwa na Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.



Akizungumza mara baada ya kukamilisha kwa ziara ya Ukaguzi wa Miradi hiyo kwa siku ya kwanza, akiwa kwenye Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Makete, Ndg. Clemence Mwawite Ngajilo, ameipongeza Halmashauri hiyo, kwa kusimamia vizuri Miradi hiyo ambayo itaenda kuwa na tija kwa Wananchi.

Aidha, Kamati hiyo ya Siasa Wilaya ya Makete, imempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. Jerry Daimon Mwaga, kwa kuielewa na kuifahamu Miradi waliyoitembelea licha ya ugeni wake, ndani ya Halmashauri hiyo.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Jerry Daimon Mwaga, amesema kuwa wamezichukua changamoto zote ambazo zimebainishwa na Kamati hiyo, na kwamba Ushauri wote uliotolewa utaenda kufanyiwa kazi ili Ilani ya CCM iweze kuetekelezwa ipasavyo.
Ikumbukwe kuwa, ziara hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Makete, CDE, Clemence Mwawite Ngajilo, ni ya Siku Mbili ambapo, leo Machi 5,2025 imekagua Utekelezaji wa Ilani katika Kata za Lupila, Mang'oto , Tandala, Lupalilo na Iwawa.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top