Katibu Mwenezi wa Baraza la wanawake la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Taifa Sigrada Mligo ameripotiwa kujeruhiwa na mlinzi wa kikao cha ndani kilichokuwa kikiongozwa na viongozi wa CHADEMA Taifa wakiongozwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche kilichokuwa kikifanyika mjini Njombe Machi 25, 2025.
Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe kupitia kwa kamanda wake wa polisi Mahamudu Banga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema,
Shambulio la kudhuru mwili alilolipata Katibu Mwenezi wa Bawacha Taifa ambaye amefahamika kwa jina la Sigrada Mligo 34, mkazi wa Mji mwema mkoa wa Njombe.