Mabaki ya mke aliyechomwa kwa magunia mawili ya mkaa sasa kuzikwa

Adimin
0

 Mabaki ya mwili wa marehemu Naomi Orest Marijani, ambaye aliuawa na mume wake Hamis Luwongo mnamo Mei 15, 2019, yanaagwa leo katika eneo la Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Baada ya kuagwa, mabaki hayo yatasafirishwa kwenda Moshi, Kilimanjaro kwa ajili ya maziko nyumbani kwao.



Tukio hili linakuja wiki chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa hukumu dhidi ya Hamis Luwongo mnamo Februari 26, 2025, ambapo Jaji Hamidu Mwanga alimhukumu kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mke wake.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, Luwongo alimuua mke wake na kisha kuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ndani ya banda la kuku katika eneo la Gezaulole, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Leo, ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika katika eneo la Mtoni Kijichi kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Naomi kabla ya safari ya mwisho kuelekea Moshi kwa maziko.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Moshi jioni ya leo au kesho alfajiri, ambapo familia na wanakijiji watampa heshima za mwisho kabla ya kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top