Waziri wa Afya, Jenista Mhaga amesema kwa kuzingatia kuwa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi hayana tiba mahususi ila mgonjwa anahudumiwa kulingana na dalili alizonazo na kufuatia kuthibitika kwa Wagonjwa wawili wa ugonjwa wa Mpox nchini, Wizara ya Afya inawasihi na kuwasisitiza Wananchi wote kuzingatia na kutekeleza afua za kujikinga ikiwemo kuepuka kugusana kwa kupeana mikono, kubusiana, kukumbatiana au kujamiiana na Mtu mwenye dalili za Mpox.
Wananchi pia wametakiwa kuwahi katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu pale Mtu anapoona mojawapo ya dalili za ugonjwa wa Mpox au kupiga simu nambari 199 bila malipo, kuepuka kuchangia vitu kama nguo na matandiko ambavyo vimetumiwa na Mtu mwenye dalili za Mpox na Mtu mwenye dalili za Mpox”
“Kuepuka kugusa majimaji ya mwili ya Mtu mwenye dalili za Mpox, kuepuka kumuhudumia mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox bila kuchukua taharadhari, Watumishi wa afya kuzingatia kanuni za kujikinga na magonjwa wakati wote wanapowahudumia wagonjwa ikiwemo wenye dalili za vipele na homa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono”
“Wizara ya Afya, itaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huu, kadri taarifa za ufuatiliaji na uchunguzi zitakavyopatikana, Wizara inashauri wananchi kuendelea na shughuli za kila siku kwa kuzingatia tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu”