Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa hafanyi mzaha kuhusu nia yake ya kutaka kugombea tena Urais wa nchi hiyo kwa mara ya tatu, pale muhula wake wa pili utakapokamilika mwaka 2029.
Hata hivyo Rais huyo mtata anajua wazi kuwa Katiba ya nchi yake hairuhusu mtu kuhudumu kwenye Urais kwa vipindi vitatu.
Akizungumza jana Jumapili kwenye mazungumzo ya simu na NBC News Trump alisema;
“Sifanyi mzaha, kuna njia ambazo unaweza kufanya ili ugombee tena,” alisema Trump lakini hakuziweka wazi njia hizo zitakazomuwezesha kufanikisha azma yake.
Maneno ya Trump yanadhihirisha waziwazi kwamba anatafuta upenyo wa kisheria utakaomuwezesha aendelee kuliongoza taifa hilo kubwa duniani kwa vipindi vitatu