Katekista auawa akituhumiwa kuchepuka na mke wa mtu

Adimin
0

 Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe limemkamata Lameck Meltus Mwamlima (29) fundi magari, mkazi wa Migombani-Tunduma kwa tuhuma za mauaji ya Vicent Daimond Mwenda (38) fundi ujenzi na pia alikuwa Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Tazara-Tunduma, mkazi wa mtaa huo aliyefariki dunia Mei 10, 2025 kwa kushambuliwa na kitu chenye ncha kali kichwani na maeneo mbalimbali ya mwili wake baada ya kuviziwa na mtuhumiwa akiwa ndani kwake amelala na kutekeleza tukio hilo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amesema kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu za mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kutembea kimapenzi na mke wake.

Aidha Kamanda Senga amesema upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top