Shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar (ZFF) limepiga marufuku kwa Klabu za mpira wa miguu kwenda Uwanjani na vikundi maalum vya kucheza vya Wanawake wanaocheza ngoma zisizo na maadili pamoja na kuvaa nguo (Vijora) na kuonekana maumbile ya miili yao.
ZFF inatoa angalizo la kuzichukulia hatua kali na stahiki kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa kwa timu zote zitakazo kaidi na kupeleka vikundi hivyo Viwanjani.