Mwanafunzi wa darasa la kwanza adaiwa kubakwa akienda shule Njombe

Adimin
0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limethibitisha kutokea kwa tukio la ubakaji dhidi ya mtoto wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 6, mkazi wa mtaa wa Ngalanga, mjini Njombe.



Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, SACP Mahmoud Banga, tukio hilo limetokea alfajiri ya Mei 22, 2025, majira ya saa moja asubuhi, wakati mtoto huyo akiwa njiani kuelekea shuleni.

Kamanda ACP. Banga amesema uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini mhusika wa tukio hili na kuhakikisha anafikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mtaa wa Ngalanga, Bw. Julius Lulandala, amesema tukio hilo limetia hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo na tayari wamechukua hatua za haraka kuimarisha ulinzi, ikiwemo kufyeka vichaka vilivyopo kandokando ya barabara ili kuondoa maficho ya wahalifu.

Ameongeza kuwa mtaa huo umeanzisha utaratibu wa kuwatambua wakazi wapya kwa kuhakikisha kila mgeni anajitambulisha kwenye ofisi za serikali ya mtaa.

"Japo hatuna ushahidi kamili, tuna hofu kuwa baadhi ya wahalifu ni waliopata msamaha wa kifungo na sasa wanafanya matukio haya ili warudi gerezani," amesema Mwenyekiti Lulandala.

Pia amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanasindikizwa shuleni asubuhi na kuchukuliwa wanaporejea jioni, pamoja na kutii marufuku ya kutembea nje baada ya saa nne usiku.

Mtaa wa Ngalanga unajulikana kwa shughuli za kilimo cha miti ya mbao, chakula na biashara. Mwenyekiti Lulanda pia ametoa wito kwa wakazi kuacha kulima mazao ya kimo kirefu kwenda juu, ambayo yanakuwa maficho ya wahalifu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top