Ushindi wa Prof Janabi,Jakaya kikwete apewa Kongole

Adimin
0

 Naibu Mwakilishi wa Kudumu Tanzania-Geneva, Balozi Hoyce Temu ambaye alikuwa kwenye Timu ya kampeni iliyoongozwa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ambayo ilizunguka Mataifa mbalimbali kumuombea kura Prof. Janabi kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa WHO- Africa, amesema Dkt. Kikwete anastahili kupewa pongezi kubwa kwa kazi nzuri iliyowezesha ushindi wa Janabi.


Kupitia taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa X  May 20,2024, Hoyce amesema “Huyu Mzee apewe maua yake kwa kweli, alimiliki jukwaa la diplomasia la kampeni ya Prof. Janabi kwa hali ya juu sana, huku mtaani tunasema Mzee alikabia juu sanaa, sisi tuliopangiwa kuwa katika timu yake tumemshuhudia akitumia mbinu nyingi na tofauti kila wakati katika kila nchi tuliyokwenda kukutana na Marais wa nchi hizo”

“Kwanza nilipopokea barua kuwa Mh. Rais Samia ameniteua kuwa katika Special Envoy na Mzee K nilipata woga sana, nikajisemea sasa hii ndio njia rahisi kabisa ya kufukuzwa kazi lakini today I must say I have no regrets maana nimejifunza mengi sana, uwezo wake wa kuzungumzia mahusiano kati ya nchi na nchi yaliwashangaza hata Marais wengine, naomba nitoe ushuhuda wa Rais mmoja alipofika kwenye kikao, alimwambia msaidizi wake kwa kifaransa; “De quoi ai-je besoin pour lui parler puisque j’ai besoin d’en apprendre davantage de lui?” akimaanisha kuwa kwani anahitaji kuongea na Mwenyekiti nini wakati yeye ndio anahitaji kujifunza zaidi kutoka kwake? , niliyojifunza kupitia special envoy ya Mwenyekiti nisingeweza kuyapata darasani kwa miaka miwili”

“Mzee K (Kama tulivyokuwa tunamuita kwenye kampeni), uwezo wake katika Diplomasia ya Kimataifa sio wa kuacha tu kusimuliwa kiwepesi hivi! najua anaandika kitabu lakini nimemuomba niweke katika kitabu ninachoandika (kuhusu kampeni tatu nilizoshiriki) na chapter yake itakuwa “Unwritten Protocols & Diplomatic Exchanges” Mungu akuweke sana Rais Mstaafu”

Itakumbukwa jana May 19,2025 wakati akizindua Sera ya Mambo ya Nje, Rais Samia alimpongeza Dkt. Kikwete kwa kuongoza ushindi wa Timu iliyopambania ushindi wa Prof. Janabi na Dkt. Kikwete ambaye alikuwa kwenye uzinduzi huo pia alimshukuru Rais Samia kwa pongezi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top