Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kusimamia vyema sera mpya ya mambo ya nje, kwa kuendelea kulinda uhuru na heshima ya taifa, hususani kupitia mabadiliko ya teknlojojia kutokana na utandawazi uliopo sasa, hivyo kuacha kugeuzwa shamba la bibi, kwa kuwapa nafasi ya watu kutoka nje ya taifa la Tanzania kuvuruga amani ya nchi.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo Mei 19, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na viongozi mbalimbali katika uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya 2001 toleo la 2024, ambayo imefanyiwa marekebisho ikiwa ni miaka 20 tangu kuzinduliwa kwa sera hiyo Aprili 30, 2001, ambapo pia ameiagiza wizara hiyo kuendelea kutoa elimu kwa watanzania na taasisi mbalimbali kuhusu sera hiyo.
Amesema kuwa Mabadiliko makubwa yametokea ndani ya Tanzania, yakiwemo ya kiuchumi yaliyoitoa nchi kutoka nchi maskini hadi kuwa nchi ya uchumi wa kati, mabadiliko katika sekta ya utalii, viwanda uchumi wa buluu, sana na michezo ambayo yameilazimu Tanzania kuifanyia mapitio sera hiyo huku eneo la mapinduzi ya teknolojia likiwa ni sehemu kubwa ya changamoto iliyopelekea marekebisho ya sera hiyo.
Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema uzinduzi wa Sera hiyo ni nyenzo muhimu ya kutetea maslahi ya Tanzania Duniani, huku utekelezaji wake ukitazamiwa kuzidi kufungua milango ya fursa na uchumi.
Akizungumza katiia uzinduzi huo wa Sera ya Mambo ya Nje, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi. Mahmoud Thabit Kombo amesema wizara hiyo itaendelea kuifanya Tanzania kuwa kuwa kisiwa cha amani, huku sera hiyo iliyoanza kufanyiwa mapitio mwaka 2021, akiitaja kama nguzo ya mikakati ya kuhakikisha Tanzania inaendeleaza na kukuza ushrikikiano wa kimataifa.