Waziri wa Madini atoa machozi jimbo lake kugawanywa...atoa ombi kwa chama

Adimin
0

MBUNGE wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Waziri wa Madini, Antony Mavunde  Mei 15, 2025 amemwaga machozi wakati akitangaza kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Mtumba iwapo atapitishwa na chama chake (CCM).

Akitoa tamko hilo kwenye mkutano maalumu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, Mavunde alisema kuwa ametafakari baada ya kusikiliza na kupima hoja mbalimbali na kuamua jambo hilo ili apate amani ya nafsi.

Alisema kuwa amepitia jumbe mbalimbali kwenye makundi sogozi ya WhatsApp ambazo zimemtia unyonge.

"Niombe tusipeleke jambo hili kwenye ushabiki na kudhihakiana, Hii ni siku ngumu sana kwangu. Natangaza Uchaguzi ujao nitagombea Jimbo la Mtumba.” Alisema Mavunde huyo huku akichukua kitambaa na kujifuta machozi.

Mavunde alisema kuwa anazo sababu kwani kwenye jimbo hilo kuna changamoto nyingi zinazogusa maisha ya watu.

Kwenye Jimbo hilo jipya la Mtumba kuna Hombolo Satellite City ambayo inakwenda kujengwa, ukiwa ni mradi wa kimkakati na pia kuna ujenzi wa Ihumwa Yard na hayo yote yanahitaji usimamizi.

"Lile ni jimbo jipya, lina changamoto nyingi zinazogusa watu wengi ili nao wafaidike na matunda ya uongozi wangu,” Alisema Mavunde na kuongeza,

"Nikipitishwa kuwa mgombea nitafanya kampeni kwenye maeneo yote na iwapo nitateuliwa nitakuwa mbunge wa wote.” Alisema.

Awali kabla ya kutangaza uamuzi huo alisema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika Jimbo la Dodoma Mjini kutokana na kuwa na miradi mingi na kuifanya Dodoma iendelee kung'ara.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma, Sophia Chibaba alisema mgawanyo wa Jimbo la Dodoma utaleta ufanisi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top