Wenyeviti wa vijiji Wapigwa msasa Makete,wapewa maagizo haya

Adimin
0

 Wenyeviti wa vijiji na vitongoji Wilayani Makete, Mkoani Njombe, wametakiwa kuwasimamia wananchi kwa kufuata sheria na maadili mema kwa jamii ili waweze kuaminika na wananchi wanaowaongoza.


Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Hamphrey Mushi wakati akifungua mafunzo ya viongozi na utawala bora yaliyofanyika Mei 15,2025, kwenye ukumbi wa Fema uliopo  Kata ya Matamba.

Aidha, Ndg.  Mushi, amewataka viongozi hao kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuwasomea mapato na matumizi ili wajue matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali pamoja na michango yao.

Kwa Upande wao Ndg. Beyond Madege na Boniface Michael kutoka chuo Cha serikali za mitaa, Hombolo kilichopo Mkoani Dodoma ,  wamewataka viongozi hao kuzingatia sheria, maadili ya kazi sambamba na kuleta mkanganyiko katika jamii.

Pia wameongeza kuwa, kiongozi yeyote wa serikali hayupo juu ya sheria, hivyo matumizi ya mabavu hayakubaliki katika jamii wanayoiongoza kwakuwa kufanya hivyo, kwani kufanya hivyo niukiukwaji wa sheria za jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Naye, Mkuu wa kitengo Cha uchaguzi wa  Halmashauri ya wilaya Makete Ndg. Kastory Ngonyani amewataka viongozi hao kujiepusha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika October 2025, huku akiwataka kuwachagua viongozi wanaokubalika na wananchi na kuwa chachu ya kuhamasisha shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Wakili Issa J Mgang,  ambae ni mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Makete, amewataka viongozi hao kuitisha mikutano na kuwasomea wananchi mapato kwa majibu wa sheria na kwamba wenyeviti wa vjiji na vitongoji hawaruhusiwi kumiliki mihuri ya Serikali kwakuwa kwa mujibu wa sheria watendaji wa vijiji ndio wenye mamlaka na wajibu wa kutunza nyaraka za serikali.

Ikumbukwe kuwa mafunzo hayo yataendelea siku ya Ijumaa ya Mei 16 2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete na yatahitimishwa siku ya jumamosi 17, 2025 katika Kata ya tandala.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top