PICHA:Ajali ya Ndege ya India yawaka Moto ikiwa na abiria 242

Adimin
0

Ndege ya abiria ya Air India iliyokuwa inatokea nchini India kwenda London nchini Uingereza imeanguka na kuwaka moto  June 12,2025 katika eneo la Ahmedabad India muda mfupi baada ya kupaa ikiwa na Watu 242.

Mamlaka nchini India zimesema ndege hiyo imebeba Watu 242 wakiwemo Wafanyakazi wa ndege hiyo 12 na tayari Timu za dharura zinaelekea eneo la tukio kutoa msaada, hadi sasa hakuna ripoti kamili kuhusu madhara yaliyojitokeza kwa Binadamu na bado sababu za ndege hiyo kupoteza mawasiliano na kuanguka haijawekwa wazi.

Ndege hiyo ni Boeing 787-8 Dreamliner yenye usajili namba VT-ANB na serial namba 36279 na ilipelekwa kuanza kazi India January 2014.

Uwanja wa ndege wa Gatwick ulithibitisha katika taarifa kwamba Ndege AI171 "ilianguka wakati wa kuondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad leo." Uwanja wa ndege ulisema ndege hiyo ilitakiwa kutua Gatwick, ambayo ni kusini mwa London, saa 18:25 p.m. saa za ndani (1:25 p.m. Mashariki).

Vituo vya Televisheni vya India vilionyesha moshi mzito ukipanda kutoka eneo la ajali, huku baadhi ya picha zikionyesha uharibifu mkubwa wa majengo na magari mengi ya kubebea wagonjwa yakikimbilia eneo la tukio.








Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top