CHADEMA Watalipia wana Ubinafsi wa Kitaasisi-Ansbert Ngurumo

Adimin
0

 Mwandishi wa habari mwandamizi, Ansbert Ngurumo, ameibua mjadala mpana kuhusu mwenendo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akikitahadharisha dhidi ya kile alichokiita “ubinafsi wa kitaasisi” na “ukanushaji wa makosa ya wazi.”


Kupitia andiko lake linalosambaa mitandaoni, Ngurumo amesema kuwa CHADEMA inaelekea kutoonesha dalili za kuvumilia upungufu wa ndani na kushindwa kujisahihisha, hata pale ambapo ushahidi na hoja dhahiri zinawekwa mezani na umma au wanachama wake wenyewe.

“Chama kinafanya kila jitihada kukwepa lawama hata kwa mambo ambayo kimekosea hadharani kwa kauli au matendo. Hakiamini kwamba kinaweza kukosea,” ameandika.

Ngurumo ameeleza kuwa hali hiyo ya kukataa kukosolewa au kupotosha mitazamo ya wakosoaji ni hatari kwa ustawi wa chama chochote kinachotaka kuaminiwa na wananchi.

“Hata pale kinapokosolewa kwa mifano hai na ushahidi, kama katika hili la "kuzuia uchaguzi," ambayo ni kauli ya mwenyekiti, kinakana. Viongozi hawataki kukiri kuwa walikosea au wanakosea”, ameongeza.

Akiwa na mtazamo wa kisayansi na wa kitaasisi, Ngurumo amefafanua kwamba mwenendo huo unaashiria hali ya organizational narcissism (ubinafsi wa taasisi), institutional denial (ukanushaji), na institutional manipulation (udanganyifu wa kimfumo).

Katika maelezo yake, amesisitiza kuwa hali hiyo ni kiashiria cha mtafaruku wa kiuongozi au kiutawala, na kwamba mashabiki wa chama hicho wanajitahidi “kutafuta huruma ya jamii kwa kupotosha maoni ya wakosoaji wao.”

Ngurumo anaonya kuwa endapo hali hiyo itaachwa bila kushughulikiwa, inaweza kuigharimu taasisi hiyo kisiasa na kijamii. Ametahadharisha pia kuwa tayari baadhi ya watu wamejipanga kumshambulia binafsi kwa kutoa maoni hayo badala ya kutafakari hoja zenyewe.

“Nayasema sasa ili kesho wasije wakatokea watu wakasema tulitelekeza taasisi, tukaiacha ifanye makosa ya wazi, tukashindwa kuishauri. Kesho si mbali. Tutakumbushana maneno haya,” ameandika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top