Wakati mchakato wa watia nia ukiendelea katika majimbo mbalimbali hapa nchini kwa nafasi ya Ubunge na Udiwani, Idawa Media tumekuandalia list ya watia nia ya ubunge jimbo la Makete Mkoani Njombe ambao tayari wameshachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
Miongoni Mwa waliochukua fomu ya Ubunge jimbo la Makete ni Pamoja na
1-Dr Toba Nguvila
Dkt Toba Nguliva aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Dar Es Salam amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe
Dkt Nguvila amechukua fomu Juni 29, 2025 katika ofisi za CCM wilaya ya Makete ambapo amesema ametimiza matakwa yanayohitajika na anakiachia Chama chake kwa hatua zinazofuata.
2-Bw. Award Mapndila
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Award Mpandila (Mchuichui) amejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe
Mpandila amejitokeza Juni 29,2025 na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Daniel Muhanza.
3- Dr Alten Ntulo
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Alten Ntulo amejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe
Ntulo amejitokeza Juni 29,2025 na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Daniel Muhanza.
4- Yeriko Kyando
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Yericko Kyando amejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe

Kyando amejitokeza Juni 29,2025 na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Daniel Muhanza.
5-Shadrack Kyando
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Shadrack Kyando ( Super Kyando) amejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe
Shadrack Kyando amejitokeza Juni 29,2025 na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Daniel Muhanza.
Shadrack Kyando amejitokeza Juni 29,2025 na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Daniel Muhanza.
Mwenyekiti wa Wanawake Tanzania Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Selina Msigwa amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge jimbo la Makete mkoani Njombe
Mpaka sasa Selina ni mwanamke wa kwanza kujitosa kwenye nafasi hiyo ya kuutaka ubunge na kufanya idadi ya watia nia waliojitokeza kuchukua fomu kufikia 6 mpaka leo saa sita mchana.
Mpaka sasa Selina ni mwanamke wa kwanza kujitosa kwenye nafasi hiyo ya kuutaka ubunge na kufanya idadi ya watia nia waliojitokeza kuchukua fomu kufikia 6 mpaka leo saa sita mchana.
7-FESTO SANGA
Mbunge wa jimbo la Makete 2020 - 2025 Festo Sanga amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
Sanga amefika ofisi za CCM wilaya ya Makete Julai 01, 2025 na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Daniel Muhanza.