Tuliripoti hapo awali kwamba Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz aliliambia shirika la utangazaji la umma la Israel Kan kwamba kama ingewezekana, wanajeshi wangemuua Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei wakati wa mzozo wa siku 12 na Tehran.
Katika mahojiano tofauti na Idhaa ya 13 ya Israel, Katz alisema watendaji wa Israel "walimtafuta sana" Khamenei, lakini hawakuweza kupata "fursa ya Oparesheni" kufanya shambulio.
Mamlaka ya Iran imeonya kuwa Israel inaweza bado inataka kumuua Khamenei licha ya usitishaji mapigano uliopo kwa sasa.
Katz pia aliiambia Channel 13 kwamba "haoni hali ambayo Iran itarejesha vifaa vya nyuklia" vilivyoshambuliwa na vikosi vya Amerika na Israeli, na kuongeza kuwa uwezo wa Tehran wa kutengeneza silaha za nyuklia "uliharibiwa kabisa".
Hata hivyo, katika hotuba yake ya kwanza tangu kusitishwa kwa mapigano, Khamenei alisema mashambulio ya Marekani "hayakusaidia lolote" kwa vituo vya nyuklia vya Iran.