Takriban watu wanane wameuawa na wengine zaidi ya 400 kujeruhiwa katika maandamano ya juni 25,2025 dhidi ya serikali nchini Kenya, mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema.
Wanane kati ya waliojeruhiwa walikuwa na majeraha ya risasi huku wengine 83 wakielekezwa kwa matibabu maalum, ilisema taarifa ya pamoja ya Chama cha Madaktari wa Kenya, Chama cha Wanasheria wa Kenya na Kikosi Kazi cha Marekebisho ya Polisi.
Maafisa watatu wa polisi pia walijeruhiwa, walisema.
"Tunawaomba wale ambao bado wako mitaani wawe waangalifu ili kuepusha maafa na majeruhi zaidi," iliongeza.
Mamlaka bado haijathibitisha majeruhi wowote.