Mwanahabari wa Njombe Tv achukua fomu kuwania Udiwani

Adimin
0

 Mwanahabari maarufu nchini Tanzania, Prosper Mfugale, ameweka wazi nia yake ya kulihudumia Taifa kwa njia ya kisiasa baada ya kuchukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani Kata ya Ihanga, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.


Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mfugale alisema kuwa uamuzi wake wa kuingia kwenye siasa unatokana na wito wa kutaka kuwatumikia wananchi kwa karibu zaidi, hasa kwa kutumia uzoefu wake katika uandishi wa habari, mawasiliano na utetezi wa haki za jamii.

“Kwa miaka mingi nimekuwa nikisikiliza na kuripoti changamoto za wananchi. Sasa ni muda wa mimi mwenyewe kuwa sehemu ya kuyatatua matatizo hayo moja kwa moja kupitia nafasi ya uongozi,” alisema Mfugale

Prosper Mfugale amejipatia heshima kubwa katika tasnia ya habari kutokana na kazi yake ya muda mrefu katika vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii, ambako alijulikana kwa uchambuzi makini wa masuala ya kijamii, kisiasa na maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wasaidizi wake wa karibu, Mfugale anatarajia kuwasilisha sera zinazolenga maendeleo ya elimu, afya, miundombinu na kuwawezesha vijana na wanawake wa Kata ya Ihanga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top