Barua inayodaiwa kutoka kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa, imeeleza kufungwa kwa shughuli za Kanisa la Ufunuo na Uzima, linalongozwa na Askofu Josephat Gwajima, kwa madai ya kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa Kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi, kwa kuwa vitendo hivyo vinaathari ya kuhatarisha amani na utulivu nchini
Pia, barua hiyo imeliamuru kanisa hilo kusitisha shughuli zake mara moja na imefutiwa usajili wake, ila lina haki ya kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ndani ya siku 21
TAZAMA VIDEO HII YA GWAJIMA