Hali ya sintofahamu imewakumba wananchi wa kijiji cha Ugabwa wilayani Makete mkoani Njombe baada ya njiwa mweupe mwenye madoa meusi na mekundu kukutwa kijijini hapo akiwa na barua inayotamka Ombeni Chaula kupewa siku 3 alipe deni analodaiwa
Tukio hilo limetokea Juni 4,2025 majira ya asubuhi ambapo barua hiyo imeandikwa kwa wino mwekundu pamoja na matone yanayodhaniwa kuwa ni damu, ambapo inamtaka Ombeni alipe deni la magunia ya mkaa aliyochukua na anatakiwa kulipa ndani ya siku 3, jambo lililozua sintofahamu kwa wananchi wa kijiji hicho.
Kwa mjibu wa taarifa iliyoripotiwa na kituo cha redio Green fm kilichopo Makete, Inaelezwa kuwa Bw, Ombeni Chauli ambaye kwa sasa hayupo kijijini hapo anadaiwa magunia hayo kweli.
Akihojiwa na Kituo Hicho Ombeni amesema kuwa hatishiki na vitisho vya njiwa huyo na kwamba hakuna jambo lolote litakalo mpata ndani ya siku tatu au ndugu zake,hivyo watu wasiwe na hofu juu ya njiwa huyo.
Taarifa za Kwa Kina unaweza Kufuatilia katika Kurasa za Kituo hicho Click here >greenfmradio