Wakili Jebra Kambole ajiondoa kesi ya CHADEMA

Adimin
0

 Wakili Jebra Kambole ametangaza kujiondoa kwenye kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA inayoendelea sasa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam



Tangu asubuhi leo, Jumanne Juni 10.2025 kumekuwa na 'mabishano' ya kisheria baina ya Mawakili wa waleta maombi na upande wa utetezi ambao ni CHADEMA iliyokuwa inawakilishwa na Wakili Jebra Kambole

Katika kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa chama hicho kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika kuendesha shughuli zake ikiwemo suala la rasmali fedha nk, hivyo kufungua maombi ya zuio dhidi ya chama hicho ya kufanya shughuli zote za kisiasa na kutumia mali za chama mpaka pale ambapo kesi ya msingi itakaposikilizwa,

Hata hivyo, inadaiwa kuwa licha ya kwamba Wakili Jebra Kambole wa CHADEMA ametangaza kujiondoa lakini Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza shauri hilo anaendelea kuendesha kesi muda huu kukiwa na Mawakili wa upande mmoja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top