Yanga Waitwa tena TFF kesho, Kamdomo kawaponza

Adimin
0

Tunapenda kuuthibitishia umma kuwa Benki ya CRDB ndiyo Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la TFF, na inatekeleza ipasavyo majukumu yake ya kimkataba.


Kwa msimu wa 2023/2024 wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Bank Federation Cup), benki hiyo ililipa fedha zote za kimkataba Tsh. TSh 255,000,000/= (Milioni Mia Mbili na Hamsini na Tano) kwa ajili ya uendeshaji wa mashindano hayo.

Tumemsikia Meneja Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC kupitia vyombo vya habari akidai kuwa klabu yao inaidai TFF Tsh. 200,000,000/= (Milioni Mia Mbili ) ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB.

Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa TFF ndiyo inayoidai klabu hiyo. Young Africans SC iliomba kwa barua fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni.

Hivyo, ili kutoendelea kusababisha sintofahamu kwa umma, tumeiandikia barua Young Africans kutuma kwetu mtaalamu wao wa fedha kesho saa 4 asubuhi kuhakiki deni la klabu hiyo akiwa na vielelezo vyote katika Ofisi za TFF.


TFF itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kusimamia mpira wa miguu ikiwemo kulinda taswira za wadhamini wake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top