Boss wa simba atoa Tamko usiku, Mashabiki hakuna kurudi nyuma

Adimin
0

Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (Mo Dewji) amesema, dhamira yake ya kuijenga Simba kuwa klabu bora barani Afrika haijabadilika. 


Bilionea huyo mwenye ukwasi mkubwa Tanzania amebainisha kuwa,tayari amewekeza zaidi ya shilingi bilioni 87 ndani ya klabu hiyo tangu mwaka 2017 ikiwa ni miaka tisa sasa imetimia.


Hayo ameyabainisha Julai 14,2025 kupitia video aliyoitoa kwa mashabiki na wafuasi wa Simba SC kupitia mitandao yake ya kijamii.

Mo Dewji amesema, licha ya changamoto mbalimbali za msimu uliopita, Simba imeonesha uimara mkubwa na kufikia mafanikio ya kihistoria.

Amesema, miongoni mwa mafanikio hayo ni kucheza fainali za CAF mara mbili ikiwa ni jambo ambalo halijawahi kufanywa na klabu nyingine kutoka Tanzania.

"Simba bado ipo kwenye hatua ya ujenzi. Roho ya ushindi haijawahi kuyumba. Tunajipanga upya kwa msimu ujao na kipaumbele kitakuwa kwenye usajili wa kimkakati na kuimarisha benchi la ufundi."

Ameongeza kuwa, mbali na uwekezaji wa mishahara, maandalizi ya timu na matumizi ya uendeshaji, pia ametoa mabilioni kama msaada wa dharura kwa klabu, jambo ambalo halipaswi kupotoshwa au kubezwa.

"Tangu mwaka 2017 hadi sasa, nimetumia shilingi bilioni 22 kwa mahitaji ya dharura pekee. Kauli kwamba Mo hatoi hela ni upotoshaji wenye malengo ya chuki."

Mo Dewji pia ametoa wito kwa wanachama na mashabiki wa Simba kuachana na maneno ya chuki na badala yake wajikite katika mshikamano, kushirikiana na kujenga klabu kwa pamoja.

"Nimewekeza muda, jasho, damu na fedha Simba. Sio kwa sababu nyingine, bali kwa mapenzi ya dhati kwa klabu hii na kwa taifa letu. Doto yangu haijabadilika."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top