Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu juu ya kutaka marejeo ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 02 wa kuahirishwa kwa usikilizwaji wa shauri la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.
Mahakama imesema maombi haya yalipaswa kusubiri kesi ya msingi iishe ndipo yawese kuwasilishwa Mahakama Kuu.
Juni 02, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam iliiahirisha shauri namba 8606/2025 la uchapishaji wa taarifa za uongo lililo chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Mhini baada ya maombi ya upande wa jamhuri kuiomba nmahakama kuwa mashahidi ambao si askari wa Jeshi la Polisi watoe ushahidi wa kificho.
Wakili Hekima Mwasipu amesema sababu za kuahirishwa kwa kesi Juni 02, hazikuwa na misingi ya kisheria. Hivyo wakataka Mahakama Kuu ipitie mwenendo wa shauri hilo.
Hata hivyo anesema wameridhishwa na uamuzi wa mahakama na shauri litakapoisha wataweza kupeleka maombi kama wakiona inabidi.
“ahirisho la tarehe mbili la kutaka kusikiliza kesi likikuwa siyo sahihi kwa sababu wao walileta sababu ambazo hazieleweki wala zilikuwa hazina misingi ya kisheria”