RC Kilimanjaro awapa Tano ZARA TANZANIA ADVENTURES Kuwa na kampeni ya Twenzetu Kileleni

Adimin
0

Na Linda Akyoo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, amezindua rasmi kampeni ya “Twenzetu Kileleni” msimu wa tano, yenye lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika ofisi za Zara Tanzania Adventure mjini Moshi, Mhe. Babu amesema kampeni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa katika kuongeza idadi ya watalii.

“Hii kampeni imekuwa maarufu sana. Tunapata wageni wengi, lakini hatuna mahali pa kuwaweka. Wito wangu kwa Mkurugenzi Zainabu, kama fedha zipo, jenga hoteli nyingine. Watalii hawana mahali pa kulala, wanapata tabu kutoka Arusha kuja Kilimanjaro,” amesema Babu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Zara Tanzania Adventure, Bi. Zainabu Ansell  amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya watalii 200 mwaka huu, wote wakipanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea uhuru wa nchi.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Anjela Nyaki, amepongeza mchango wa Zara Tanzania Adventure katika kukuza utalii na kuongeza mapato ya taifa kupitia idadi kubwa ya watalii wanaowaleta kila mwaka.

Zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro linatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 hadi Desemba 10, 2025, likiwa pia ni sehemu ya kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hususani Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.










Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top