Muumini atuhumiwa kumuua mchungaji wake baada ya maombi

Adimin
0

 Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia Victor Thomas, mkazi wa kitongoji cha Kadudu Kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi, kwa tuhuma za mauaji ya mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Thomas Nkasimongwa,mkazi wa Kijiji cha Lupaso.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema tukio hilo limetokea Juni 27, 2025 katika Kijiji cha Lupaso mtaa wa Misheni.

Amesema siku ya tukio, mtuhumiwa akiwa na ndugu zake walikwenda kanisani kwa ajili ya kuombewa kutokana na changamoto inayomkabili mtuhumiwa huyo na baadae waliamua kumrejesha nyumbani kwa ajili ya kuendelea na maombi wakiwa na mchungaji huyo (marehemu).

Walipokaribia nyumbani kwa mtuhumiwa, mtuhumiwa huyo aliruka kwenye pikipiki na kukimbilia ndani na kisha kutoka na panga na kuanza kumkimbiza mchungaji na kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake, na hivyo kusababisha kifo chake.

Mtuhumiwa huyo ni muumini wa kanisa hilo la TAG na amekuwa akipata huduma ya kuombewa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kamanda Issa Suleiman amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top