Kwa Mujibu wa Takwimu kutoka katika Tovuti ya StatCounter iliyotolewa leo July 13, 2025, Mtandao wa Facebook unaomilikiwa na Kampuni ya @meta Umetoa Mialiko ya Watumiaji wa Tanzania zaidi ya 64,915 kujiunga na Programu yao Mpya inayoitwa "Content Monetisation" ambapo Mwenye Account ataweza kunufaika na content zake atakazopost katika Account yake.
Programu ya Content Monetisation inajumuisha Story, Post za Picha, Video, Maandishi na Short-clips (Reels). Ambapo Mtu ataweza kujiingizia Pesa kutokana na Nguvu yake ya Kupost either Story, Picha, Video ndefu, Maandishi au Video fupi (Reels), Ikiwa content creator atafikisha kiwango kuanzia dollar 100 (Tshs 257,000) ataweza kutoa Pesa na kwenda katika Kadi yake ya Benki au Kwa Njia ya Paypal.
Ikumbukwe Mpaka Kufikia Mwezi June, kwa Mujibu wa StatCounter, facebook ilikuwa imetoa Mialiko 3,290 pekee kwa Content creators wa Tanzania. Hii inamaanisha kuna Ongezeko la takribani Account 61,625 zinazolipwa na mtandao wa Facebook nchini Tanzania kwa Mwezi Julai.
Mtandao wa Facebook Umetoa Taarifa pia kupitia Jukwaa lake la Watengeneza Maudhui (Facebook for Creators) kuwa Utaendelea kutoa Mialiko zaidi na zaidi kwa Account zote zinazofanya vizuri, zenye maudhui bora na yenye Ushawishi mpaka kufikia August 31 Mwaka huu.
Ili kubaini Ikiwa Account yako imepewa mualiko ingia katika Professional Dashboard, elekea katika Monetisation kisha Angalia neno "Content Monetisation" ikiwa mbele utaona neno "SETUP" fahamu umepewa Mualiko huo.
Je, Account yako inakuingizia Chochote? 😀 Tuandikie katika sehemu ya Maoni.
Usisahau unaweza kuni FOLLOW kupata updates zaidi #justinemtasiwa #justinemitumba