Soma mpaka mwisho, kisha SHARE na wenzako!
Katika pitapita zangu, nimekutana na video ya Cardi B akieleza jambo zito kwa sisi watengeneza maudhui mtandaoni.
👉 Mwanzo ukiwa unaanza, watu wengi hawakupi kipaumbele.
👉 Baadaye wanavutiwa kidogo, wanaanza kufuatilia na hata kukushabikia.
👉 Ukifika hatua fulani, wanakuwa upande wako kwa nguvu.
Lakini… ukianza kuvuka “level” waliyoizoea, hapo ndipo vita huanza!
Wengine wanakupiga vita, wanakutukana, wanakudhalilisha. Hapo ndipo wengi hukata tamaa.
Cardi B alisema kwake vita hivyo vilidumu miaka 3–4! Wengine hukata tamaa mapema, lakini ukivumilia na kusonga mbele, sehemu ya waliokuwa wakikupiga vita watarudi na kukuunga mkono zaidi kuliko mwanzo.
Somo kubwa ni hili:
🔥 Kukutana na vita ni ishara umefika level ya juu.
🔥 Kinachokumaliza sio vita, bali jinsi unavyovitikia.
🔥 Siri ya mafanikio ni kuwapuuza na kusonga mbele.
Mimi mwenyewe nilipitia vipindi hivi. Nilitukanwa, kuzushiwa, kuombewa mabaya, hata mipango mibaya kufanywa dhidi yangu. Nilikaa kimya, nikachukua hatua pale ilipohitajika kisheria, na nikaendelea na safari yangu. Baadaye baadhi waliorudi walikiri walikosea.
Hivyo, content creator yoyote anayepiga hatua lazima apitie vita.
Ukija kuvipitia, usitetereke. Usitumie nguvu zako kupigana nao – hiyo ndiyo wanayotaka. Endelea na mstari wako, na utaona jinsi wanavyopotea mmoja mmoja.
⚡ Kumbuka:
Vita hivi siyo vya kukumaliza – ni vya kukujenga. Mungu huwatumia watu hawa kukuweka imara, bila wao kujua.
🙌 Kama wewe ni mtengeneza maudhui, chukua ujumbe huu kama silaha ya kukupa moyo. Endelea kutembea, endelea kuumba, na tufanye dunia iwe sehemu salama ya kuishi.
👉 Kama ujumbe huu umekugusa, SHARE na wenzako!