Na Linda Akyoo ;Dodoma.
Ikiwa ni Muendelezo wa Wiki ya Huduma kwa wateja ,Mamlaka Ya maji safi na Usafi wa mazingira dodoma (DUWASA) Wamefika katika Mtaa wa Mlimwa C Uliopo Jijini Dodoma Leo tarehe 08 Oktoba,2024 Kuwasikiliza wananchi na wateja wa mtaa huo,Ambapo wametoa malalamiko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutopata maji kwa wakati na kuingiziwa bili ilihali hawapati huduma ya maji
Akijibu malalamiko ya wateja hao Mkurungezi wa huduma kwa wateja Duwasa Bi Lena Mwakisale Amesema Suala la kusomewa Bili ya maji kwa wateja ni la Kila mwezi na Haki ya mteja kushirikishwa wakati wa usomaji wa Mita ya maji
Aidha Bi.Mwakisale Ameongeza kwa kuwaomba wananchi pindi wanapopata ujumbe wa Bili wakasome kwenye Mita zao ili kujua kama Bili iliyotumwa inauhalisia
Sambamba na hilo asema Kuwa Duwasa inatambua changamoto hiyo ya upungufu wa maji na wapo katika hatua nzuri ya kuhakikisha wananchi wa mtaa wa Mlimwa C wanaunganishwa kwenye bomba kubwa lililopo maeneo ya wajenzi.