Na Linda Akyoo -Moshi.
Waziri wa Afya Mhe.Jenista Mhagama ameuagiza uongozi wa Shule ya Sekondari Dkt Asha Rose Migiro iliyopo Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kuotesha miti katika shule hiyo ili wanafunzi wa shule hiyo wapate mazingira mazuri,Safi na bora ya kujisomea.
Waziri Mhagama ameyasema hayo tarehe 07 Oktoba,2024 kwenye ziara ya kutembelea Shule hiyo ambapo ameweza kukaguwa majengo mapya ya madarasa na mabweni ya kidato cha tano na chasita.
Aidha Mhe Mhagama amsifu mradi huo wa madarasa pamoja na mabweni na kusema kuwa"huu umekuwa mradi namba moja kati ya miradi yote niliyo itembelea".
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro,Mhe Nurdin Babu, amesema kuwa pamoja na kwamba Mhe Waziri anashughulikia Afya lakini ameweza kutembelea miradi mingine kama vile Shule ambayo Mhe Raisi ameleta pesa nyingi za maendeleo jumla ya Bilioni 915 zimeletwa mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Dkt.Asha Rose Migiro Bi.Flaviana Sumawe ameishukuru serikali kwa kuongeza shule hiyo kwa kidato cha tano na chasita na kusema ukimwelimisha mwanamke umeelimisha Taifa zima.
Shule ya Sekondari ya Dkt Asha Rose Migiro ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wanafunzi 361,shule ilipokea shilingi Milioni 429 kwaajili ya upanuzi wa kidato cha tano na chasita,huku lengo likiwa ni kutoa elimu kwa mtoto wa kike wa Kitanzania.